Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

MO Salah aivuruga Misri

Дата публикации: 26-09-2026 10:42:59

NYOTA wa Misri na Trabzonspor, Mohamed Salah ameondoka kwenye kambi ya timu ya taifa huku kukiwa na taarifa za mvutano katika kikosi hicho baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Angola katika mechi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Основное содержимое страницы с новостью.

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Communications Limited

Cairo, Misri: NYOTA wa Misri na Trabzonspor, Mohamed Salah ameondoka kwenye kambi ya timu ya taifa huku kukiwa na taarifa za mvutano katika kikosi hicho baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Angola katika mechi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Salah, ambaye ni nahodha wa timu hiyo, alitolewa dakika ya 60 na Kocha Hossam Hassan, uamuzi ambao umeibua maswali miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka Misri.

Baada ya mechi hiyo, Hassan alisisitiza kumtoa Salah hakukutokana na majeraha, bali ulikuwa uamuzi wa kiufundi. Kocha huyo hakutoa dalili nyota huyo alikuwa na tatizo lolote la kiafya.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Misri, Ahmed Abdel Basset, Salah ameondoka kambini kwa utulivu huku akikwepa kuhusishwa na mgogoro wowote unaodaiwa kuibuka katika kikosi.

Taarifa hizo zinaeleza kumekuwa na hali ya sintofahamu ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo, huku baadhi ya kauli zilizotolewa baada ya mchezo dhidi ya Angola zikichochea zaidi mjadala kuhusu kinachoendelea katika kikosi hicho.

Sare hiyo imeongeza presha kwa Misri, ambayo ilitarajiwa kuanza kampeni yake ya kufuzu AFCON 2027 kwa ushindi ikiwa nyumbani au ugenini dhidi ya Angola. Badala yake, ilishindwa kupata bao katika dakika zote 90.

Hassan sasa anakabiliwa na jukumu la kurekebisha mambo ndani ya timu kabla ya mchezo wake unaofuata dhidi ya Sudan Kusini, unaotarajiwa kuchezwa Septemba 29.

Mchezo huo utakuwa muhimu kwa Misri katika harakati zake za kuwania tiketi ya AFCON 2027, lakini pia utakuwa kipimo kwa Hassan kuhusu namna atakavyodhibiti hali ndani ya kikosi chake.

Wakati huo huo, macho yataelekezwa kwa Salah na kama atarejea kambini au kutoa maelezo zaidi kuhusu sababu za kuondoka kwake. Hadi sasa, hakuna maelezo rasmi kutoka Shirikisho la Soka Misri kuhusu hatua hiyo.

Kwa sasa, taarifa za mvutano ndani ya kambi zimeongeza presha kwa Hassan, huku Misri ikihitaji ushindi dhidi ya Sudan Kusini ili kurejesha hali nzuri katika kampeni yake ya kufuzu AFCON.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Rais wa CAF afunguka ishu ya Afcon 2027 kuondolewa Tanzania02019-09-2026
2Gamondi amtaja aliyeiua Stars011.6726-09-2026
3Tanzania: Afcon 2027 Preps On Course010.4125-09-2026
4Ufunguzi Kombe la Dunia 2026 Mexico08.0712-06-2026
5Ahmedy Ally aipiga mkwara Yanga mastaa wa Simba wakienda Sauz kwa makundi,jeuri ya MO Dewji01025-09-2026
6Nigeria/Madagascar: Nigeria Vs Madagascar Preview - Super Eagles Begin Race to Afcon 2027 in Uyo010.8625-09-2026
7Mbappé aumia goti, kuikosa mechi ya Ubelgiji05.8926-09-2026
8Mhilu mambo safi Geita Gold011.526-09-2026
9Baleba njia yake Man United yahitaji subira08.0625-09-2026
10Nigeria/Madagascar: 2027 Afcon Qualifiers - Five Madagascar Players That Can Shock the Super Eagles011.3425-09-2026

Классификация: Спорт. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 7.92. Источник: www.mwanaspoti.co.tz.