Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

FEROOZ: Miaka 21 ya 'Starehe' na bado unaishi

Дата публикации: 24-09-2026 11:46:55

MSANII wa Bongo Fleva, Feruzi Mrisho Rehani 'Ferooz' amesema kila anapopanda jukwaani na kuimba wimbo wa Starehe unakuwa na mapokeo makubwa kama ameuandika hivi karibuni, wakati una miaka zaidi ya 21.

Основное содержимое страницы с новостью.

By  Olipa Assa

Reporter

Mwananchi Communications Limited

MSANII wa Bongo Fleva, Feruzi Mrisho Rehani 'Ferooz' amesema kila anapopanda jukwaani na kuimba wimbo wa Starehe unakuwa na mapokeo makubwa kama ameuandika hivi karibuni, wakati una miaka zaidi ya 21.

Ferooz aliliambia Mwanaspoti namna miaka 30 ya Bongo Fleva inavyowakutanisha na jamii pamoja na mashabiki wao, jinsi inavyowapa picha ya jamii bado inahitaji kusikia ujumbe unaowagusa moja kwa moja.

"Mfano wimbo wa Starehe ulikuwepo katika albamu ambayo niliitoa mwaka 2004 ingawa mimi kimziki nimetoka 2003, katika tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva iliyofanyika Arusha ni wimbo ambao ulikuwa na vaibu kubwa ya mashabiki na ndiyo uliyonilipa zaidi," amesema Ferooz na kuongeza;

FER 01

FER 01

"Kitu ambacho kinanishangaza wimbo unatumika katika masuala mbalimbali ya mambo ya afya, wakati mimi mwenyewe mhusika sihusishwi, pia nilitegemea hata maazimisho ya Ukimwi duniani, wangekuwa wanashirikiana na mimi katika kutoa elimu ila haijawa hivyo.

"Kupitia miaka 30 ya Bongo Fleva nimepata picha ya kuandika ujumbe zaidi ambao utaendelea kuishi katika jamii, kama zilivyo nyimbo zangu zingine kama Wema, Nakaza Roho, ambazo mara nyingi zinatokana na uzoefu wa maisha ya kila siku ya jamii.

FER 02

"Jukwaa la miaka 30 ya Bongo Fleva, haliishi tu kuwapa kipato wasanii, bali linalenga kurejesha maadili ya muziki pia jamii iendelee kutuona ni mfano wa kuigwa,hivyo tuna kazi ya kutenganisha feki na halisi," amesema Ferooz ambaye alitumia miezi sita kuandika wimbo wa Starehe kabla ya kurekodi hadi kuandaa video.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Staa wako Bongo naye ana staa wake mamtoni09.3726-09-2026
2Singeli 'kichaka' kinachompa maisha D Voice06.4826-09-2026
3Ran Kida: Kutoka Kagera hadi kutawala majukwaa ya dance Tanzania01023-09-2026
4Basata yamshushia rungu Dudu Baya, mratibu wa Bongo Flava 30010.3426-09-2026
5Rany Kida; King of Dance mwenye simulizi moto ya dansi09.0724-09-2026
6Любимые племяшки ❤️ Феде сегодня исполнилось 7 лет 🎉 Он ...09.8226-09-2026
7Dili jipya la Curry Warrios sio mchezo010.426-09-2026
8Lamine: Mbappe na mimi ndo bora zaidi duniani08.4425-09-2026
9Ahmedy Ally aipiga mkwara Yanga mastaa wa Simba wakienda Sauz kwa makundi,jeuri ya MO Dewji01025-09-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 9. Тональность: 0. Информативность: 10.39. Источник: www.mwanaspoti.co.tz.